Nyanza FlashINVITATIONS
EnglishAnza sasa

KWA WATU WAKO. KWA SIKU YAKO.

Siku yako
ya kipekee.
Ianze na mwaliko.

Kabla ya muziki, maua na kumbukumbu—kuna mwaliko. Wakaribishe watu wako kwa kadi yenye hadithi yako, kisha simamia wageni kwa urahisi.

Fungua mfano bila akaunti · Tumia simu au kompyuta

Bibi na bwana harusi wakisherehekea kwenye bustani kando ya ziwa
Mwanzo wa kumbukumbu nzuri.
TUNAKUALIKAAmina &
Joseph
Pamoja na watu tunaowapenda.
KARIBU TUSHEREHEKEEMfano wa mwaliko
KILA SABABU YA KUSHEREHEKEA

Harusi Send-off Kitchen party Mahafali

ZAIDI YA KADI NZURI

Mwaliko wenye hisia.
Mipango yenye utulivu.

Uzuri unaoonekana kwa mgeni. Mpangilio unaokusaidia nyuma ya pazia. Kila kitu muhimu kwa mwaliko wako, sehemu moja.

Kadi inayoeleza hadithi yako

Weka picha, majina na taarifa za tukio. Mgeni afungue mwaliko wake binafsi kwenye simu.

Jua nani anakuja

Fuatilia majibu ya RSVP na panga orodha ya wageni wako kabla ya siku yenyewe.

Mapokezi yanayoenda vizuri

Tumia QR kuthibitisha mwaliko na kurekodi walioingia wakati wa mapokezi.

TUKIO LAKO, HISIA ZAKO

Kuna mengi ya kusherehekea.

Chagua mtindo wa kadi

KARIBU NI ZAIDI YA NENO

Wageni wajisikie
sehemu ya siku yako.

Kutoka kwenye mwaliko wenye jina la mgeni hadi mapokezi mlangoni. Punguza kufuatilia taarifa sehemu tofauti, uwe na muda wa kufurahia maandalizi.

  • Shiriki link ya mwaliko binafsi
  • Fuatilia RSVP kwenye akaunti yako
  • Rekodi wageni walioingia kwa QR
Ona anachopokea mgeni
Meza za wageni zilizopambwa kwa maua na mishumaa
GN
Grace NdaloMgeni wa Amina & Joseph
RSVPNitahudhuria
Mapokezi Mwaliko umethibitishwa
Mfano wa taarifa za mgeni

ANZA NA WAZO LAKO

Kutoka wazo
hadi “karibu”.

Huhitaji kuwa designer. Anza na mtindo unaoupenda, ongeza taarifa zako na hakiki mwaliko kabla ya kuutuma.

01

Chagua na tengeneza

Fungua akaunti, chagua aina ya tukio na mtindo wa kadi. Weka majina, picha, tarehe na eneo.

02

Ongeza wageni na shiriki

Andaa orodha yako ya wageni. Hakiki kadi na gharama za huduma ulizochagua kabla ya kutuma.

03

Fuatilia na karibisha

Angalia majibu ya wageni na tumia QR kwenye mapokezi. Taarifa zako zibaki pamoja hadi siku ya tukio.

NA KWA MIPANGO YA PAMOJA

Michango nayo iwe na mpangilio.

Rekodi ahadi na malipo ya michango kwenye akaunti yako, ili uwe na kumbukumbu iliyo wazi ya maandalizi.

Anza kupanga

KABLA HUJAANZA

Maswali machache.
Majibu rahisi.

Invitations inatoa huduma gani?

Nyanza Flash Invitations husaidia kutengeneza cards, kusimamia wageni na ujumbe wa event, RSVP, mapokezi kwa QR na kumbukumbu za michango. Huduma ya kutuma SMS za biashara zinazojitegemea iko sms.nyanzaflash.com.

Mgeni anahitaji akaunti au app kuona kadi?

Hapana. Mgeni anaweza kufungua link ya card kwenye browser ya simu au kompyuta. Akaunti inahitajika kwa mwenye event kusimamia kadi na wageni. Unaweza pia kufungua sample kabla ya kuanza.

Bei ya card inajumuisha SMS na WhatsApp zote?

Si lazima. Card/template/design na gharama za channels zinaweza kuwa vipengele tofauti. Idadi ya recipients, segments na huduma ulizochagua huathiri jumla. Kagua breakdown iliyoonyeshwa kabla ya confirmation; bei ya SMS standalone haitumiki moja kwa moja kwa kila huduma ya Invitations.

Invitations inaweza kutuma ujumbe wa kawaida?

Ndiyo, ikiwa ujumbe unahusiana na card, event au register ya michango husika. Unaweza kutuma taarifa na reminders kupitia sehemu ya huduma hiyo. Invitations si huduma tofauti ya general bulk SMS; kampeni za biashara zisizohusiana na event zitumie SMS system.

Angalia FAQ zote

Furaha ya wanandoa kwenye sherehe ya harusi

WATU WAKO WANASUBIRI MWALIKO

Ianze kwa mwaliko.
Ibaki kuwa kumbukumbu.

Tengeneza mwaliko wako